Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa
1
2
3

Andika kichwa cha kampeni yako

Hili ndilo jambo la kwanza watu watakaloona kuhusu kampeni yako. Nasa umakini wao kwa mada fupi ambayo inaangazia mabadiliko ambayo ungependa waunge mkono.

Tafadhali andika kichwa cha habari.

Endelea

Ifanye fupi na inayolenga ndipo

Mfano: "Piga marufuku Mifuko ya Plastiki jijini Nairobi"

Makinikia suluhisho

Mfano: "Virusi vya Corona: Funga shule zote Dodoma"

Onyesha udharura wa suala

Mfano: "Saidia kulinda Vifaru Weusi walio hatarini kutoweka"

Chagua mtoa-maamuzi

Huyu ndiye mtu, shirika au kikundi ambacho kinaweza kufanya uamuzi kuhusu kampeni yako.

Tafadhali ongeza mtoa-maamuzi unayemlenga.

Endelea

Chagua mtu ambaye anaweza kukupa unachokitaka

Huenda akawa meya wa jiji lako ikiwa ni kuhusu kufunga shule, au serikali yako ya kitaifa ikiwa unaomba likizo ya aliyeugua yenye malipo.

Usiende moja kwa moja hadi kileleni

Unaweza kupata matokeo ya haraka zaidi ukichagua mtu wa ngazi ya chini kidogo ambaye hulengwa mara chache kuliko wale wanaotambulika.

Chagua mtu ambaye unaweza kufanya kazi naye

Kampeni yako ina uwezekano mkubwa wa kushinda kwa kufikia makubaliano na mtoa-maamuzi wako.

Eleza tatizo unalotaka kusuluhisha

Aghalabu watu wataunga mkono kampeni yako ikiwa ni wazi kwa nini unalijali suala lenyewe. Eleza jinsi mabadiliko haya yatakavyokuathiri wewe, familia yako, au jamii yako.

Tafadhali ongeza maelezo.

Fafanua kuhusu watu wanaohusika na shida inayowakabili

Wasomaji huwa na msukumo zaidi wa kuchukua hatua ikiwa wanaelewa ni nani aliyeathiriwa.

Fafanua kuhusu suluhu

Elezea ni nini kinahitajika kufanyika na ni nani anayeweza kufanya mabadiliko. Weka wazi kile kitakachotokea ikiwa kampeni itashinda au kuambulia patupu.

Ibinafsishe

Kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa wasomaji watatia saini na kuunga mkono kampeni yako ikiwa ni wazi kwa nini unalijali suala hili.

Waheshimu wengine

Usiwadhulumu wengine, kutumia matamshi ya chuki, kutishia vurugu au kuyaunda mambo yasiyo ya kweli.

Hakikisha kuwa maelezo yako ni sahihi

Usahihi wa mambo ni muhimu! Kutia kampeni saini ni kitendo cha imani, na kuhakikisha kuwa kampeni yako ni sahihi ni mojawapo ya masharti ya kutumia tovuti hii. Kwa vidokezo vya kukagua ukweli, tazama hapa.​