Tanzania: Acha kuwafukuza Wamasai
Kwa Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mawaziri na Mamlaka za Uhifadhi nchini Tanzania:
Kama raia kutoka duniani kote, tunakuomba upinge jaribio lolote la kuwafukuza Wamasai kutoka katika ardhi yao ya asili au kuwalazimisha kuhama ili kupisha wawindaji wanyama kutoka nchi za nje.
Tunakutegemea kuwa mtetezi wa watu wako na kuzuia jaribio lolote la kubadilisha haki zao za ardhi kinyume na matakwa yao.
Weka anwani yako ya baruapepe:
Watia sahihi wa hivi karibuni
Kwa Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mawaziri na Mamlaka za Uhifadhi nchini Tanzania:
Tunakutegemea kuwa mtetezi wa watu wako na kuzuia jaribio lolote la kubadilisha haki zao za ardhi kinyume na matakwa yao."
Sisi ni wazee wa kabila la Wamasai kutoka Kaskazini mwa Tanzania. Siku yoyote kutoka sasa , maelfu kwa maelfu ya watu wa jamii yetu wanaweza kulazimishwa kuondoka kwenye ardhi zetu za jadi ili kupisha utalii wa kiwango cha juu, uwindaji, na biashara ya kaboni.
Tunahitaji msaada wako haraka sana.
Miaka iliyopita tulipokabiliana na vitisho kama hivi, zaidi ya wanachama milioni 2 wa Avaaz walijiunga na wito wetu! Pamoja, tulitengeneza kimbunga kikubwa kiasi kwamba Rais wa zamani aliahidi kamwe hatotaka kutufukuza kutoka kwenye ardhi zetu.
Lakini sasa, mipango mikubwa ya kutufukuza inarejeshwa! Rais Samia Suluhu Hassan anaweza asitusikilize sisi, lakini tunajua ataitia shinikizo la umma na vyombo vya habari - kwenu nyote!
Jiunge nasi sasa - na sambaza kampeni hii kwa wingi ili kumwonyesha kuwa dunia inasimama na Wamasai!
- Wazee wa Wamasai wa Tanzania pamoja na Avaaz.
TANBIHI: Picha iliyotumika haihusiani na wazee wa Wamasai nchini Tanzania wanaotuma ombi hili, kwa ajili ya kuhakikisha usalama wao.
Ilichapishwa:
Waambie Marafiki zako