

Sitisha kuwaondoa wapiga kura wa Wamasai!
Kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Tanzania:
Tunakuomba urejeshe mara moja haki za kupiga kura kwa raia wote Wamasai wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi katika tarafa ya Ngorongoro. Lazima uache mara moja kuwafukuza kwa nguvu, ulinde ardhi na haki zao za eneo na urejeshe huduma zote za kijamii.
Weka anwani yako ya baruapepe:
Watia sahihi wa hivi karibuni
Kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Tanzania:
Raia 100,000 wa kimasai wameondolewa kutoka kwenye orodha za wapiga kura nchini Tanzania, kwa sababu ya ujasiri wao wa kuamua kubaki kwenye ardhi za mababu zao. Kwa kutumia bunduki na mabomu ya machozi, serikali imewafukuza maelfu ya Wamasai asilia ili kupisha utalii wa safari. Sasa, wanachukua hatua nyingine ya kuumiza zaidi kwa kuwanyima wachache wajasiri waliobaki nyumbani katika wilaya ya Ngorongoro haki yao ya kupiga kura.
Serikali ya Tanzania inajaribu kulificha jambo hili ili kuepuka kukosolewa na wafadhili wanaounga mkono demokrasia - lakini kelele kubwa ya kimataifa kutoka kwa harakati yetu inaweza kusababisha kujulikana kwa ukiukaji huu wa haki za binadamu, kuwafanya wafadhili watoe masharti, na kusaidia Wamasai kupata tena haki yao ya kupiga kura.
Uchaguzi unakaribia kwa kasi - ongeza jina lako sasa:
Waambie Marafiki zako