Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa

Msaada

Jinsi Kampeni Zetu Zinavyofanya Kazi

Muhtasari wa kampeni fanifu ya mtandaoni


ANZA KWA WAZO ZURI


Kila kampeni kuu huanza kwa wazo zuri. Ni mambo gani unatamani yangekuwa tofauti na ambayo unaweza kubadili ikiwa patapatikana shinikizo la kutosha?

JIAMINI


Uzoefu, hisia, na uangavu wako utakuelekeza vyema zaidi ya unavyokadiria. Iwapo unahisi kuwa jambo fulani si la haki na linaweza kuchukuliwa hatua, kuna uwezekano mkubwa kwamba wengine watakubaliana nawe.

ZINDUA KAMPENI KATIKA HATUA TATU RAHISI


Kugeuza wazo lako kuwa harakati kuu ni rahisi kama 1, 2, 3 ukitumia jukwaa la Kampeni za Jumuiya ya Avaaz! Hizi hapa hatua:
  1. Anza: Jaza maelezo ya msingi kuhusu kampeni -- unataka nini, unamuuliza nani, na kwa nini?
  2. Chapisha: Kagua kampeni yako kabla ya kuichapisha kwenye tovuti, hariri chochote ungependa kubadilisha kisha ubonyeze kuchapisha ili watu waweze kuitia saini.
  3. Shiriki: Kila kitu ki tayari. Sasa, eneza habari -- kampeni yako haitajitia saini yenyewe!

Hamu ya kuanza imekuzidi? Bofya hapa ili kuunda kampeni sasa!
https://www.avaaz.org/kampeni_za_jumuiya/sw/zindua_kampeni/

JUHUDI JUU YA JUHUDI


Ukishakwisha kuiunda kampeni yako, ni kuingia mbioni kukusanya saini.
Bofya hapa ili kupata vidokezo kuhusu jinsi ya kufanya hivi kwa ufanisi:
https://www.avaaz.org/kampeni_za_jumuiya/sw/kuza_kampeni_yako/

WASILISHA KAMPENI YAKO


Unapokuwa tayari kuwasilisha kampeni yako, hakikisha inagonga ndipo kwa kishindo kwa mlengwa au mtoa-maamuzi uliyemchagua. Jambo rahisi zaidi kufanya ni kutuma baruapepe inayotoa maelezo ya kampeni pamoja na orodha iliyotiwa saini kisha ufuatilie kwa simu ili kuhakikisha kuwa mlengwa aliipokea baruapepe yako. Lakini usiogope kuwa mbunifu -- hujawekewa vikwazo vyovyote kuhusiana na unayoweza kuyafanya na kampeni yako! Vinginevyo tafakari kuiwasilisha kampeni ana kwa ana, kuandaa mkutano, kufanya onyesho fulani ili mlengwa aitilie kampeni maanani au ili kupata usikivu wa vyombo vya habari, na chochote kinginecho unachoweza kufikiria.

KAZA KAMBA


Kuwasilisha kampeni yako mara moja kunaweza kutosha kutwaa ushindi -- lakini huenda ikawa sivyo. Kwa wengine, ni hatua ya kwanza pekee katika kampeni pana. Lifikirie suala lenyewe kutoka kwa mtazamo wa mlengwa wako -- je, ungalikuwa wao, ni nini kingekufanya uchukue hatua? Labda ni kuwasilisha kampeni ana kwa ana kwa njia yenye makeke zaidi, au kukusanya saini nyingi zaidi ili kuiweka wazi hoja yako kwa nguvu zaidi. Au labda wangeliwajibikia suala iwapo lingekuwa kwenye habari, ambapo unaweza kufanya juhudi ili kampeni yako iangaziwe katika vichwa vya habari.