Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa

Msaada

Kuunda Kampeni Itakayoshinda

VIDOKEZO VYA KUFANIKISHA KAMPENI

Katika kipindi cha miaka 5 iliyopita, Jumuiya ya Avaaz imeshinda kampeni nyingi kupitia harakati za mtandaoni. Na ingawa kila kampeni ni ya kipekee, hizi hapa ni baadhi ya sifa ambazo kampeni zilizoshinda zinazo kwa pamoja. Mafunzo makuu kutokana na harakati za Avaaz yametandazwa hapa chini.

Kuubadilisha ulimwengu kumerahisishwa zaidi.

ZINAVYOFANYA KAZI KAMPENI ZETU
Mchakato wa hatua kwa hatua wa kuchukua wazo na kuligeuza kuwa mabadiliko ya kisiasa kupitia kampeni ya mtandaoni.

KUIPA KAMPENI YAKO KICHWA
Kichwa ndicho sehemu ya kwanza ya kampeni yako ambayo watu wataona -- na isipokuwa ya kunasa, huenda ikawa ya mwisho! Jifunze jinsi ya kuifanya kampeni yako iwe ya kipekee kwa kutumia kichwa kinagonga ndipo.

KUANDIKA MAELEZO YA KAMPENI
Hii ndiyo hoja ya msingi inayoeleza kwa nini watu wanapaswa kutia saini na kwa nini mlengwa achukue hatua -- iboreshe ili ifanikiwe iwezekanavyo kwa kujumuisha vipengee muhimu kutoka kwa kampeni nyingine zilizoshinda.

KUWEKA SHABAHA YA KAMPENI
Kampeni yako itakuwa thabiti kadri matakwa yako yalivyo madhubuti. Hakikisha kuwa umeweka matakwa ya kuridhisha kwa kuzingatia viashiria hivi muhimu.

KUCHAGUA M(WA)LENGWA
Kuchagua vizuri utakaposhindilia shinikizo kunaweza kukurahisishia ushindi zaidi. Soma vidokezo hivi ili kuchagua mlengwa au mpokeaji bora zaidi wa kampeni yako.

KUCHAGUA PICHA
Picha ina thamani ya maneno elfu. Ipe kampeni yako fursa ya kusema zaidi kwa kutumia picha yenye ushawishi mkubwa.

KUIENEZA KAMPENI YAKO
Nguvu ya kampeni yako hutoka kwa idadi ya watu wanaoitia saini. Zaidi ya watu milioni 14 wameziunga mkono kampeni za Avaaz katika muda wa miaka michache. Soma kuhusu njia za kuipa kampeni yako kani kuu zaidi hapa.