Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa

Msaada

Kuandika Kichwa cha Kampeni

Kuyasema yote kwa vibambo visivyozidi 100


Kichwa ndiyo sehemu ya kwanza ya kampeni watakayoona watu -- na isiponasa umakini wako, huenda ikawa ndiyo ya mwisho! Ndio maana ni muhimu sana kutumia maneno machache yaliyo wazi, ya kuvutia, na yanayobainisha kiini cha kampeni vilivyo. Hii hapa mifano na mapendekezo kadhaa ya kuimarisha kichwa cha kampeni yako.

VIDOKEZO:

  • Jumuisha “meme” yako: yaani kifungu cha maneno au misemo ya mtandaoni inayojipachika kwenye kumbukumbu, inasemeka kwa urahisi na inapakia habari tosha.
    Mifano ya "meme": Almasi za damu, kilio cha msaada Tibet, watu kabla ya faida
  • Ifanye mahususi: Unaweza kumtaja mlengwa, kubainisha ni kipengee gani cha sheria kampeni yako inaangazia, pamoja na jiji au nchi husika.
  • Tumia vitenzi halisi: Kifanye kitendo kuwa kitu ambacho kila mtu atataka kujiunga nacho.

MIFANO:

  • Kenya: Komesha Sheria itakayaoiangamiza Misitu!
    Ni bayana kuhusu mahali na sheria mahususi inayolengwa, wakati ule ule ikiwavutia watu wasio na habari kuhusu aidha ya mambo haya.
  • Mwalimu Mkuu Mwanga: Acha kukataa kuuidhinisha Muungano wa Wanafunzi
    Imetumia maneno ya utendaji na kuangazia matakwa ya kampeni kama uamuzi ambao mlengwa anaweza kuufanya.
  • Mwondoe Michael Gumzo mamlakani
    Hapana kupiga gumzo, ni ya moja kwa moja -- imetumia maneno ambayo yanaweza kurejelewa katika kampeni nzima, yanayoelezea lengo la harakati kwa njia mpya na inayosalia katika kumbukumbu.
  • Nassetta, Mkurugenzi Mtendaji wa Hilton: ekomesha ubakaji katika hoteli zako
    Imemzungumzia mlengwa moja kwa moja, huku ikimhusisha na jambo la kushtua na kutatanisha.
  • Jibu kilio cha msaada cha Tibet, komesha ukandamizaji wa Uchina
    Hii ni bayana na vilevile inaibua maswali fulani -- unaelewa kwamba Watibet wanahitaji usaidizi dhidi ya ukandamizaji wa Wachina, lakini hujui kilio cha msaada ni kipi hasa au vipi tunaweza "kukijibu".
  • Mwambie Waziri wa Mazingira wa Umoja wa Kongo: "Ni kufanya Hila au kufanya Hima" katika sera yetu ya misitu?
    Ucheshi au utani kidogo unaweza kusaidia pakubwa.