Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa

Msaada

Kuchagua picha

Wacha picha zikusaidie kunena

Picha inayofaa inaweza kusema yote pindi tu inapotupiwa jicho. Picha za kampeni zinaweza kuifanya kampeni yako kuwa ya kusisimua, kuvutia umakini wa watu, na kuwapa motisha ya kuchukua hatua. Hivi hapa vipengee mahususi vya picha za kampeni, zikiwa zimechaguliwa kutoka kwa mamia ya mifano na majaribio:

1. REJELEA UBINADAMU WETU -- MWANGAZIE MTU FULANI


Maelezo ya taabu kuu ya kiuchumi barani Ulaya yanaweza kukosa kueleweka kwa urahisi, na umati wa waandamanaji unaweza kuwa ndiyo habari kuu badala ya kile wanachokifanyia maandamano. Kwa kumtia msichana kwenye darubini, picha hii inaleta akilini jinsi maamuzi ya kiuchumi yatakavyoathiri maisha yake ya baadaye pamoja na ndoto zake.2. IAKISI KAMPENI


Kiini cha kampeni hii ni wanavyoumia watoto kupitia unyanyasaji usio na maana na wa kizamani wa mabomu ya nguzo -- na hilo linaonekana bayana katika picha yenyewe.3. ONYESHA UPEO WA TATIZO


Salalaa! Miti hiyo inaonekana mikubwa kwelikweli na kuna mingi sana iliyokatwa. Picha hii inadhihirisha kiwango cha uharibifu wa mazingira unaofanyika nchini Brazili na kulifanya jambo linalotukia mbali -- kuangamizwa kwa msitu wa Amazoni -- kuwa kitu halisi (na ambacho ungependa kukomesha!).4. MJUMUISHE MLENGWA WAKO


Kuiweka taswira ya mlengwa wako kama picha ya kampeni ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa analihisi joto la shinikizo kibinafsi -- hamna anayependa kukosolewa hadharani.5. IFANYE YA KUPENDEZA MACHO


Rangi na mwanga katika picha hii zinavutia vilivyo -- halaiki ya watu walio na rangi nyekundu, ya chungwa, na manjano inazua hisi ya staha inayowasilisha nguvu na uchangamfu.6. ONYESHA UKINZANI


Unapoitazama picha hii tu, unahisi kuwa hali hii haifai -- polisi waliovalia magwanda ya kutuliza ghasia wakiwasukuma wanawake, watoto na hata mkembe aliye uchi. Ulinganisho wa makundi hayo mawili unastaajabisha na unaonyesha dhuluma iliyopo ikiwa ni pamoja na tofauti kali kati ya wanaoandamana na jinsi serikali inavyoyajibu maandamano hayo.7. KUTUMIA UTAMADUNI WA KISASA KUJITANGAZA


Chukua ishara au jambo fulani ambalo kila mtu analitambua na ulibadili ili liakisi ujumbe wa kampeni yako.8. PICHA ZA KUOGOFYA SIO BORA VILE


Picha za kutisha na kuogofya au kuatua moyo, ingawa huzua hisia kali, zinaweza kutibua makini ya watu kutoka kwenye kampeni au kuwafanya watake kuuondokea ukurasa upesi. Picha hii maridadi ya tembo wakubwa iliisaidia kampeni ya kupinga ujangili zaidi ya picha ya ndovu anayefuja damu baada ya kuuawa.