Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa

Msaada

Jinsi ya kuuthibitisha ukweli wa kampeni yako

Kwa nini nahitaji kuthibitisha ukweli?

Kutia kampeni saini ni kitendo cha imani. Ni sharti kwamba taarifa zote zinazowasilishwa kwenye jukwaa la Kampeni za Jumuiya ya Avaaz ziwe za kweli na sahihi. Sharti hili limetiliwa mkazo na kuwekwa bayana wakati wa mchakato wa kuunda kampeni na katika viwango vyetu vya maudhui.

Jinsi ya kuukagua ukweli wa kampeni yako

TUMIA VYANZO VINAVYOAMINIKA

Fanya utafiti mtandaoni ili kupata vyanzo vya kuaminika kwa kila dai unalotoa, kama vile hati rasmi na makala ya habari kutoka vyombo vya habari vinavyoaminika. Mambo yanayowasilishwa na mashirika ya vyombo vya habari yenye tajiriba ni ya kuaminika zaidi kuliko yanayopatikana kwenye blogu ya mja asiyejulikana, tovuti ya mambo mahususi, chapisho la mitandao ya kijamii. Hii ni kwa sababu vyombo vya habari vya kitaaluma vinajali uaminifu wake na vina taratibu za kuuhakiki ukweli.

NI MAONI AU NI UKWELI

Ukweli ni taarifa zinazoweza kuthibitishwa. Maoni ni maelezo ya hukumu au imani ya mtu. Katika mfano huu; “Kijiji chetu kina duka linalouza aiskrimu ya mdalasini, ninayoipenda” kuna mambo mawili ya hakika, yakifuatwa na jambo moja ambalo ni maoni.

EPUKA KUTOA MADAI USIYOWEZA KUTHIBITISHA

Kwa mfano, epuka kusema, “Ujenzi wa barabara kuu mpya utaua tembo wote”, ikiwa hakuna ushahidi wa kuiunga mkono kauli hii. Badala yake, fikiria kuelezea wasiwasi wako kulingana na maoni yako au ya wengine. Kwa mfano: “wataalamu kutoka Idara ya Wanyamapori wamesema makazi ya tembo yatakatwa vipande viwili na barabara kuu, hivyo kupunguza eneo lao la kupekua na kupata chakula”. Au, “Barabara kuu mpya huenda ikatishia maisha ya tembo, kwa vile wanahitaji kusafiri kutafuta chakula.”

HAKUNA VYANZO VYA UMMA VINAVYOPATIKANA?

Ikiwa hupati hati za umma au taarifa za habari zinazoaminika ili kuunga mkono maelezo yako, basi jiulize ni kwa nini. Je, una uhakika kuwa maelezo unayowasilisha ni sahihi? Una ushahidi gani? Hakikisha kuwa umeweka vyanzo vyako wazi kabisa kadri uwezavyo. Ikiwa ni kitu ulichoshuhudia, kwa mfano, sema hivyo, na utoe maelezo mengi uwezavyo. Na litumie jina lako halisi, isipokuwa pale unapokuwa na sababu maalum ya kutofanya hivyo (ni jina la kwanza na herufi ya kwanza ya jina la ukoo pekee zitakazoonekana kwenye tovuti).

Huu hapa mfano wa kampeni iliyothibitishwa:

 

Komesha uchimbaji wa mafuta kwenye ufuo maridadi wa Algarve!

Algarve huvutia mamilioni ya wageni [1] kwa fuo zake za kupendeza, chakula murua, na hali ya anga mwanana [2]. Eneo hili hutegemea utalii [3], ambao unategemea kudumisha mazingira safi na bahari safi.

Kampuni ya mafuta ya ENI/Galp ilipewa leseni [4], kinyume na matakwa ya raia [5], kuchimba katika njia ya uhamiaji ya pomboo na nyangumi, bila utafiti wa athari za kimazingira kufanywa [6]. Na ni eneo lenye hatari kubwa ya mitetemeko ya ardhi [7].

Sisi ni wanabaharia, si wasafishaji wa mafuta. Huu ni uhalifu utakaotutibukia baadaye - kama vile tukio la kutatanisha la Ghuba ya Meksiko - tafadhali tusaidie kuukomesha!


VYANZO:

[1] Kweli: Mnamo 2016, Algarve ilipokea zaidi ya watalii milioni 4
https://en.wikipedia.org/wiki/Tourism_in_Portugal
https://www.ine.pt/ngt_server/attachfileu.jsp?look_parentBoui=299820007&att_display=n&att_download=y

[2] Dai hili halihitaji kuthibitishwa, kwa vile si la ukweli usiopingika. Iwapo tunakiona kitu kuwa kizuri, cha kuvutia, kibaya au kinachofaa, ni suala la maoni.

[3] Kweli: Utalii ndio tasnia kuu huko Algarve:
https://ec.europa.eu/growth/tools-databases/regional-innovation-monitor/base-profile/algarve-region-portugal-0

[4] Kweli: ENI/Galp ilipewa leseni ya kuchimba mafuta kwenye pwani ya Algarve:
http://www.theportugalnews.com/news/algarve-oil-drilling-approved/45624

[5] Je, mwandishi anaweza kudai kuzungumza kwa niaba ya watu wote? Katika suala hili, ndio: Palikuwepo na mashauriano ya umma kuhusu hitaji la utafiti wa tathmini ya athari. Asilimia 100 ya umma ulioshiriki mashauriano, au jumla ya watu 42,000, waliunga mkono kufanywa kwa utafiti, ambao hatimaye HAUKUFANYWA na wakala wa mazingira:
https://www.dn.pt/lusa/interior/petroleo-lpn-indignada-subscreve-receios-de-plataforma-algarve-livre-de-petroleo-9352627.html

- Ripoti ya hatima inaweza kupakuliwa hapa kwenye "Relatório de Consulta Pública":
http://participa.pt/consulta.jsp?loadP=2160
- RTA, Mkoa wa Kitalii wa serikali ya Algarve, pia ulipinga uchimbaji bila utafiti wa tathmini ya athari:
https://www.dn.pt/lusa/interior/petroleo-avanco-do-furo-sem-estudo-poe-em-risco-habitantes-do-algarve---turismo-9351924.html
- Miji 16 ndani ya eneo hilo ilipinga vibali hivyo vya kuchimba visima:
https://www.dn.pt/lusa/interior/municipios-do-algarve-criticam-governo-e-pedem-fim-da-prospecao-de-petroleo-9110491.html

[6] Kweli: Serikali ilivitoa vibali bila utafiti wa athari za mazingira:
https://algarvedailynews.com/news/14246-no-environment-impact-assessment-needed-oil-drilling-to-go-ahead-off-aljezu

[7] Kweli: Algarve na Lisbon ndiyo maeneo yaliyomo katika hatari zaidi ya mitetemeko ya ardhi nchini Ureno:
http://www.theportugalnews.com/news/new-study-shows-algarve-and-lisbon-are-most-prone-to-earthquakes-as-small-tremor-hits-faro/40939