Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa

Msaada

Kumchagua Mlengwa wa Kampeni

Kuelekeza kampeni yako kwa mtu anayefaa


Mlengwa ni mtu unayempa changamoto hadharani na moja kwa moja ya kuchukua hatua. Kuchagua mlengwa mwafaka kunaweza kuwa ndiyo tofauti kati ya kampeni inayofaulu na kampeni ambayo hata haijulikani kuwa ipo. Lakini kuamua ni nani utakayemlenga aghalabu huwa kugumu. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ya kuzingatia unapomchagua mlengwa:

KUHUSU MLENGWA:


  • Mlengwa wako anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya uamuzi unaoutarajia. Ikiwa anahitaji idhini kutoka kwa mtu aliye juu yao, basi zingatia kumlenga mtu huyo badala yake. Mtu anayesimamia ununuzi katika kampuni ya fanicha huenda akahitaji mkubwa wake kuidhinisha mpango wa kubadili kanuni na kutumia mbao ambazo asili yake si misitu ya mvua. Unapojipata huwezi kufanya uamuzi wa hakika kati ya walengwa wawili, ni bora zaidi kumlenga mtu mwenye mamlaka, cheo au uwezo wa juu zaidi.
  • Mlengwa anapaswa kuwa mtu binafsi, si kikundi au shirika fulani. Kwa hivyo utamlenga mwenyekiti wa kamati muhimu ya Bunge, sio 'Bunge'; Meya, sio 'jiji'; Mkurugenzi Mtendaji, sio kampuni yenyewe. Ni barabara kabisa kuwalenga watu kadhaa, kama vile washiriki wawili ambao hawajafanya uamuzi wao katika baraza la jiji.
  • Mlengwa ni binadamu. Ana hisia, malengo ya kitaaluma, marafiki, familia na jamaa, na kila kitu ambacho watu wengine wanacho. Fikiria jinsi mambo haya yanavyoweza kuathiri uamuzi wao juu ya suala lako na ni nini muhimu kwao. Ikiwa unajua kuwa mtu huyo anapanga kustaafu mwaka ujao, hataki kuchaguliwa tena lakini anaweza kujali sana wasifu wake.

MASWALI YA KUZINGATIA:


Ni uamuzi wa nani unahitajika ili kuafiki matakwa ya kampeni?
  • Kampeni yafaa kumlenga mtu ambaye ana mamlaka au uwezo wa kukidhi haja yako.
  • Mlengwa anapaswa awiane moja kwa moja na suluhu mahasusi unayoipendekeza.

Je, mtu huyu atajibu?
Watu wenye mamlaka kuu mara nyingi ndio wagumu zaidi kuwafikia.
  • Kwa kampuni: Mkurugenzi Mtendaji anaweza kuwa mlengwa mwafaka, lakini huenda akuwa na shughuli mzo mzo. Ingawa mlengwa wako anapaswa kuwa mtoa maamuzi, unapaswa kuwasiliana na watu wengine katika kampuni, kama vile waliopo katika idara ya uhusiano wa umma, ili kuhakikisha kuwa una mtu anayekusikiliza na ambaye anaweza kumfikia mtoa maamuzi.
  • Kwa serikali ya kitaifa: Rais huwa na mamlaka mengi, lakini hahusiki katika maamuzi mengi nchini. Je, suala lako ni muhimu vya kutosha kuwa kwenye ajenda yake? Labda waziri au mbunge ndiye chaguo mwafaka.