Sahihisha Mipangilio yako ya Vidakuzi ili kutumia kipengee hiki.
Bofya 'Ruhusu Vyote' au washa 'Vidakuzi vya Kulenga' tu
Kwa kuendelea unakubali Sera ya Faragha ya Avaaz ambayo inafafanua jinsi data yako inaweza kutumiwa na jinsi inavyolindwa.
Nimeelewa

Msaada

Kuweka Lengo la Kampeni Yako

Kuwa na matakwa madhubuti ni nusu ya ushindi


Ule usemi "tahadhari kwa unayotaka na kutamani" pia unahitaji kuzingatiwa katika kampeni. Matakwa ya kampeni yako ni kipengee kipaumbele katika uwezekano wako wa kushinda; ufunguo wa mlango wako wa ushindi tunaweza kusema -- matakwa bora huvuta ushindi, ilhali yale yasiyofaa huufanya ushindi kuwa muhali. Hivi hapa vidokezo rahisi vya kukusaidia kuandaa madai madhubuti ya kampeni yako.

Teua suluhu


Mara nyingi kuna njia nyingi za kutatua suala fulani. Kwa mfano, unaweza kuzuia mashirika kuwashawishi wanasiasa kwa kupitisha sheria inayoweka kipimo cha michango kwa wagombeaji, kuwashawishi wagombeaji kukataa michango kwa hiari, au kwa kuyauliza mashirika yaache kutoa michango. Hakikisha unazitafakari suluhisho mbalimbali za tatizo unalotaka kushughulikia na uchague lililo bora zaidi -- aghalabu hilo huwa lile linaloweza kukupatia ushindi pasi na wewe kutoa jasho jingi.

Ifanye mahususi


Lengo zuri ni lililo wazi, linalokadirika, na thabiti. Iwapo hutabainisha kile unachotaka vilivyo, itakuwa rahisi zaidi kwa mlengwa wako kujifanya amekupa uliyotaka bila kufanya hivyo hasa. Pia inamaanisha kuwa ni vigumu zaidi kujua unaposhinda. Ikiwa unaiomba serikali iweke mshahara utakaokimu mahitaji ya kila mmoja vyema lakini ukose kuweka wazi ni kiasi gani kinachohitajika, huenda usijue kama nyongeza ya asilimia 10 inayopitishwa inakupa kibali cha kutangaza ushindi.

Yaandae matakwa yanayoweza kukupa ushindi


Matakwa yako yanapaswa kuwa mambo ambayo yanaweza kufanyika katika hali halisi na ambayo mlengwa wako ana uwezo au mamlaka ya kuyatekeleza. Kubadilisha sheria ya jimbo si jambo ambalo mkuu wa shule yako anaweza kulifanya, lakini anaweza kuwa na mawazo kuhusu jinsi ya kulitekeleza.

Fahamu ukweli


Si lazima uyafafanua maelezo yote hadharani, lakini ni vyema kujua ya kutosha kuhusu kile unachouliza. Kwa mfano, huenda ukabananga juhudi tele ukikakamilia mkakati ambao tayari upo lakini haujatekelezwa. Je, kuna maeneo mengine ambayo yana mikakati sawia? Mbona mlengwa wako hajafanya hivi kufikia sasa, bila wewe kumwuliza? Je, unatarajia mlengwa wako aijibu vipi kampeni yako?